Nimepata taarifa kutoka kwa watu walio karibu na Lowasa kuwa tangu juzi
chakula hakijapanda kwa mzee. Kwamba kila akiwekewa chakula mezani,
anachokonoa kidogo tu na inachukua muda mrefu kati ya tonge moja hadi
jingine. Pia mdau huyo kanidokeza kuwa Mzee Lowasa kwa sasa ana mawazo
mengi sana na hajui afanye nini. Wapo waliomshauri kuwa akae kimya
katika kipindi hiki kigumu ili apate muda wa kutosha kutafakari na
kufanya maamuzi. Hata hivyo, ushauri huo ameutupa kwani anahisi kwamba
muda ukipita atasahaulika na yale aliyopanga kuyatekeleza hayatatimia.
Wapo waliomshauri kwamba aende kwao Monduli akatulie japo kwa wimbi
mbili na asiruhusu watu wamtembelee ili mawazo yake yapungue. Wapo pia
wanaomshauri kuwa aende kwenye vyombo vya habari na kueleza kwa nini
amekatwa. Wanaomshauri hivyo wanaona kuwa hiyo ndo njia sahihi kwani
kukaa kwake kimya kunaacha sintofahamu kwa wapenzi wake.
Hata hivyo, nimetafakari sana juu ya hatma ya Lowasa na nimebaini kuwa anasumbuliwa na mambo yafuatayo;
1. JINSI YA KUREJESHA FEDHA ZA WAFADHILI WAKE
Lowasa ametumia kiasi kikubwa cha fedha tangu aanze mchakato wa kwenda
Ikulu, vyanzo vyangu vimebaini kuwa Lowasa ametumia zaidi ya shilingi
bilioni 50 hasa kuanzia mwaka 2012 alipojitokeza hadharani kuchangia
huduma za kijamii, mashirika ya kidini, watu binafsi na taasisi
mbalimbali. Kati ya fedha hizo, shilingi bilioni 30 zimetumika kwa
kipindi cha 2014 hadi alipokatwa rasmi Julai 9. Inaelezwa kuwa kiasi
kingine cha fedha kipo mikononi mwa watu na kingine hakijulikani
kimeenda wapi ijapokuwa bill imeenda kwa Lowasa. Hiki ni kiasi kikubwa
cha fedha. Ni fedha ambazo alipewa kwa wafadhili wake kwa mategemeo kuwa
zitarejeshwa baada ya yeye kwenda Ikulu ambapo walikubaliana kuwa
watapewa miradi ya serikali. Hata hivyo, baada ya kukatwa, Lowasa hana
namna tena ya kurejesha fedha hizo. Baadhi ya wafadhili wake kama akina
Karamagi, Rostam, Manji na Reginald Mengi wameanza kumnunia na kwamba
tangu juzi, baadhi yao hawajapiga hata simu kumsalimia tofauti na hapo
awali ambapo kila mara walikuwa wanapiga simu kujuliana hali na
kubadilishana mawazo. Jambo hili linamtatiza sana Lowasa.
2. HATMA YA MAISHA YAKE BAADA YA KUKATWA.
Lowasa alikuwa na uhakika wa asilimia 100 kuwa ndiye Rais ajaye. Ubongo
wake aliutune usipokee aina nyingine ya maisha tofauti na majukumu ya
mkuu wa nchi. Kitendo cha kukatwa hata kabla ya kuingia tano bora,
hakika kinamnyima raha sana.
3. KUKIMBIWA NA WATU WALIOKUWA KARIBU NAYE.
Baadhi ya watu ambao mara zote walikuwa karibu naye inasemekana kuwa
wamemkimbia. Miongoni wa watu hao ni pamoja na Emmanuel Nchimbi, Hamisi
Mgeja, Jerry Slaa, Sophia Simba, Adam Kimbisa, Apson Mwang'onda, Mohamed
Abdulaziz, Kingunge Ngombale Mwiru, Msukuma na wengineo wengi. Eneo
ambalo amepoteza watu wengi ni kanda ya ziwa ambako aliwekeza fedha
nyingi. Hakika kitendo cha watu hao kumkimbia ni pigo kubwa sana kwake.
Sasa anakumbuka msemo wa kiswahili kwamba mgaa gaa namupwa hali wali
mkavu. Kumbe waru wale hawakuwa na mapenzi mema kwake na kilichokuwa
kinawapeleka ni fedha zake tu. sasa bahari imekauka wameamua kuikimbia
lwani na kwenda kuishi bara.
4. MATAMSHI YA BAADHI YA WAFUASI WAKE KUMUUNGA MKONO MAGUFULI.
Baadhi ya wafuasi wake wamenukuliwa wakitoa matamshi ya kumuunga Mkono
Mgombea wa CCM, JOHN POMBE MAGUFULI. Miongoni mwao ni Emmanuel Nchimbi
ambaye ndiye alimuandaa kuwa Waziri Mkuu wake. Watu hao wamesikika
wakisema kuwa hawana budi kumuunga Mkono Magufuli kwa vile anauzika
kuliko wagombea wengine waliochukua fomu. Maneno hayo yamemkasirisha
sana Lowasa na yanaendelea kumtesa kila akisoma kwenye mitandao ya
kijamii. Ina mana yeye Lowasa hauziki?
5. WANACHAMA WALIOMDHAMINI WAKATI WA KUOMBA RIDHAA YA CHAMA
Lowasa alipata wadhamini zaidi ya laki nane na hivyo kuwa kinara kuliko
wagombea wengine. Mgombea aliyepata wadhamini wachache, Magufuli ndiye
kaibuka kuwa mshindi. Hilo linamtesa sana Lowasa. Kinachomsumbua zaidi
ni zile pesa alizotumia kuwapa wadhamini hao. Lowasa anajua kuwa
wadhamini hao wanajua siri hiyo na wakati wowote wataiweka hadharani.
Ikiwa siri hiyo itawekwa hadharani, ni wazi kuwa ataendelea kuumbuka na
hata kama atahama chama, huko atakakoelekea hatakuwa wa maana tena.
Kuna orodha ya mambo mengi sana yanayomtesa Lowasa. Hata hivyo, kukaa
kimya anaona kuwa siyo suluhisho kamili. Njia anayoona muafaka ni ile
aliyotumia awali. Yaani kuitisha press conference na kutoa ya moyoni.
Yaani kati ya wagombea wote 38 waliorejesha fomu, huyu pekee ndiye
anayeteseka baada ya kukatwa. Wengine wametulia tulii na wamekubaliana
na matokeo. Hata hasimu wake kisiasa Benard Membe na hata Sammuel Sitta
wameamua kukaa kimya na kutokuwa waropokaji. Wameheshimu maamuzi ya
vyombo halali vya chama vilivyoundwa kwa kazi hiyo. Kazi ya KUKATA
waliochukua fomu kwa vile masharti ni kwamba kuwe na wagombea watano tu
wanaoenda NEC.
Kwa kumalizia, nawakumbusha Msemo wa JK kwamba UKITAKA KULA KUBALI NA
WEWE KULIWA. Ndicho kinachomtesa hasa Lowasa. Kala sana vya watu na sasa
anahofia kuliwa. Anajua kuwa watu kama akina Karamagi, Manji, Rostam
hawatakubali kuona fedha zao zimeteketea. Lazima zirudi kwa njia yoyote
ile.
0 comments:
Post a Comment