Friday, August 7, 2015

Star wa Bongo Flava Africa Naseeb ‘diamond’ Abdul, na mpenzi wake Mganda Zarina ‘Bosslady’ Hassan wamefanikiwa kupata mtoto wa kike alfajir ya August 6 jijini Dar Es Salaam.
Stars kadhaa pamoja na uongozi wa Icon huyu, wamejitokeza kuwapongeza wapenzi hawa kwa hatua ya kujenga familia yao.
Picha kadhaa zinaendelea kusambaa mitandaoni kufafanua tukio hilo, mtoto huyo amepewa jina la Latifah.
Wakati furaha hii ikiendelea, tayari ndani ya masaa 8 binti huyu ameanza kupokea ‘deal’ ya matangazo kutoka kwenye maduka mbalimbali nchini.
Meneja wa kimataifa wa Diamond, Sallam Sk ametusanua kupitia twitter kuhusiana na kuendelea kupokea ‘michongo’ ya matangazo.

Tuesday, July 28, 2015

wa  Nini  UKAWA  Wameamua  LOWASSA  Awe  Mgombea  wao  wa  Urais??..... Tundu  Lissu  Amelijibu  Swahi  hili  kwa  Ufasaha  Kabisa  hapo  chni:

Edward Lowassa anajiunga na CHADEMA na atakuwa mgombea urais wa CHADEMA na wa UKAWA. Lowassa is perhaps the most controversial and divisive political figure in the country right now.

Na amekuwa hivyo kwa muda mrefu. Sisi CHADEMA tulimweka kwenye Orodha ya Mafisadi kutokana na kuhusika kwake na Kashfa ya Richmond mwaka 2007.

Kwa hiyo swali halali kabisa ambalo lazima tulijibu kwa ufasaha ni hili: kwa nini tumekubali, sio tu kumpokea kama mwanachama, bali kumpa heshima ya kuwa mgombea wetu wa urais.

Na kwa nini washirika wetu wa UKAWA nao wamemkubali kuwa mgombea wao wa urais??? Jibu ni kwamba tupo katika kipindi na mazingira ya kipekee ya kisiasa katika nchi yetu. Kwa mara ya kwanza katika historia yetu kama taifa, tunaona mfumo tawala ukipasuka vipande vipande.

Kwa mara ya kwanza tunaona CCM ikipasuka katikati. Na mtu aliyeipasua CCM na mfumo tawala ni Edward Lowassa. Sisi CHADEMA tumefanya kazi kubwa ya kujenga chama tangu 2010.

 Tuna wagombea wengi na bora katika majimbo mengi ya uchaguzi na ngazi ya madiwani kuliko ambavyo tumewahi kuwa nao kwa miaka yote ya nyuma. Hata hivyo, ni ukweli pia kwamba kuna maeneo mengi ya nchi ambako tuko dhaifu sana.

Kwa kuingia kwake CHADEMA na UKAWA, Lowassa anayaingiza maeneo hayo kwenye ulingo wa kisiasa and very much within our reach.

Na Lowassa ataiporomosha CCM kwa sababu ana nguvu kubwa ndani ya chama hicho kuliko mwanasiasa mwingine yeyote. Katika mazingira ya sasa ya kipekee, tunahitaji kuamua nani ni adui mkubwa zaidi wa nchi yetu na ustawi wake:Edward Lowassa mtuhumiwa wa ufisadi au CCM na mfumo tawala ambao unajenga mazingira yanayostawisha na kulinda ufisadi.??

Sisi Chadema na UKAWA tumeamua kuwa adui yetu mkubwa wa sasa na siku zote ni CCM na mfumo tawala.

Tumemkaribisha Edward Lowassa kwa sababu kuwepo kwake kutaharakisha kuiangamiza CCM na mfumo tawala. Tunaomba wananchi mtuelewe na kutuunga mkono.


Wednesday, July 22, 2015




DAANG

Loyiso kijana wa miaka 19 ameweka headlines kubwa sana jijini Johannesburg South Africa baada ya tukio la janga la treni kutokea mjini hapo.
Kijana huyo aliyekuwa kwenye kipindi cha mitihani alifariki siku ya jana baada ya kuthubutu kucheza mchezo wa kurukaruka ndani na nje ya treni iliyokuwa kwenye spidi kali, mchezo unao hatarisha maisha.
Train SA1
     

Loyiso alikuwa njiani kuelekea shule wakati mchezo huo ulipogeuka kuwa tukio la kutisha, baadhi ya abiria waliokuepo kwenye treni hiyo walisema…
>>> “alikuwa anarukaruka ndani na nje ya treni hii na kwa bahati mbaya aliteleza na kuingia katikati ya reli za treni tukiwa tunakaribia kituo cha Chiawelo Railway Station”.<<<
TRAIN SA2

>>>walikuwa kikundi…kikundi cha vijana waliokuwa wanacheza mchezo huu, lakini kwa bahati mbaya huyo mmoja aliteleza na kuingia chini ya reli ya treni na kichwa chake kilisagwa. Ni tukio la kutisha sana na linavunja moyo.<<<
Vyombo vya kulinda usalama kwenye kituo cha Chiawelo Railway Station vimekuwa vikijaribu kupambana na tatizo la mchezo huu kwa muda mrefu sana kwani limekuwa tishio kwa jamii. Tukio hili limewaacha ndugu, jamaa, marafiki pamoja na wanafunzi wengi na masikitiko makubwa.
Nimekusogezea video inayoonyesha jinsi mchezo huu unavyochezwa nchini South Africa.

>>>walikuwa kikundi…kikundi cha vijana waliokuwa wanacheza mchezo huu, lakini kwa bahati mbaya huyo mmoja aliteleza na kuingia chini ya reli ya treni na kichwa chake kilisagwa. Ni tukio la kutisha sana na linavunja moyo.<<<
Vyombo vya kulinda usalama kwenye kituo cha Chiawelo Railway Station vimekuwa vikijaribu kupambana na tatizo la mchezo huu kwa muda mrefu sana kwani limekuwa tishio kwa jamii. Tukio hili limewaacha ndugu, jamaa, marafiki pamoja na wanafunzi wengi na masikitiko makubwa.
Nimekusogezea video inayoonyesha jinsi mchezo huu unavyochezwa nchini South Africa.



Tuesday, July 21, 2015

Msanii jembe wakilishi la Tanzania{Bongo}Diamond Platnumz anayeendelea kumake headlines kila kukicha kwenye Media tofauti kutokana na uwezo wake kuzidi kukuwa kimataifa,
Hii ni baada ya Diamond kuwa mshindi wa tuzo bora za muziki Africa{MTV MAMA AWARDS 2015} kwenye kipengele cha mtumbuizaji bora wa kiume kwa mwaka 2015.
Kupitia ushindi huo imani imezidi kuwa kubwa kwa Wabongo,haswa baada ya kutangazwa kugombea kwenye vipengele vingi katika tuzo nyingine za AFRIMMA AWARDS 2015.
ANGALIA VIPENGELE ANAVYOSHINDANIA HAPO CHINI,
      1. Best Artist Of the Year
2. Best Dance Video (Nana)
3. Best Video (Ntampata Wapi)
4. Best East Artist of the Year
5. Best Collaboration (Nana)
6. Song of the Year (Ntampata Wapi)
7. Best Inspiration Song: Alive by Bracket ft Diamond platnunz & Tiwasavage...
These is the Recently Video Music From South Africa Artist DONALD and our Beloved Diamond Platnumz From Tanzania, This song Called "WANGU" DIRECTED BY: Justin Campos

Monday, July 20, 2015

Rais wa UEFA toka 2007, Michel Platini, ameombwa na wadau wengi wakubwa wa soka agombee nafasi ya Urais wa Fifa...Platini amesema anasupport ya Confederation yake na Asia, Marekani ya Kaskazini, Visiwa vya Caribbean, Marekani ya Kusini na Marekani ya Kati...Sepp Blatter ambae anaondoka ataanzisha mjadala wa mabadiliko ya Fifa na atakutana na executive committee kuhusu tarehe ya uchaguzi wa Fifa lakini Confederatin nyingi wangependelea tarehe 6 Desemba iwe siku ya uchaguzi...Bofya hapa upate habari zaidi  
Kocha wa Manchester United Louis Van Gaal amezoeleka kuwa aina ya kocha ambaye hapendi masikhara toka kwa wachezaji wake na amekuwa si mzito kufanya maamuzi ya kumuondoa mtu kwenye timu pale ambapo anaona anakwenda kinyume na matarajio yake . Hilo lilidhihirika siku chache zilizopita wakati ambapo kocha huyo alipotangaza wazi kuwa na mpango wa […] The post Kocha Manchester United amfukuza kipa. appeared first on Maimu love