Friday, August 7, 2015

Star wa Bongo Flava Africa Naseeb ‘diamond’ Abdul, na mpenzi wake Mganda Zarina ‘Bosslady’ Hassan wamefanikiwa kupata mtoto wa kike alfajir ya August 6 jijini Dar Es Salaam.
Stars kadhaa pamoja na uongozi wa Icon huyu, wamejitokeza kuwapongeza wapenzi hawa kwa hatua ya kujenga familia yao.
Picha kadhaa zinaendelea kusambaa mitandaoni kufafanua tukio hilo, mtoto huyo amepewa jina la Latifah.
Wakati furaha hii ikiendelea, tayari ndani ya masaa 8 binti huyu ameanza kupokea ‘deal’ ya matangazo kutoka kwenye maduka mbalimbali nchini.
Meneja wa kimataifa wa Diamond, Sallam Sk ametusanua kupitia twitter kuhusiana na kuendelea kupokea ‘michongo’ ya matangazo.

0 comments: